Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 DESEMBA 2023

12 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunamulika mchango wa vijana katika mkutano wa COP28.  Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo vita Gaza, na hudam ya afya. Mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyosaidia wafugaji kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

  1. Katika saa za mwisho za mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 majadiliano yanaendelea kwa matumaini kwamba wajumbe watatoka na makubaliano yatakayoweka ulimwengu kwenye njia ya mustakabali endelevu zaidi. Hata hivyo rasimu ya awali ya makubaliano hayo inaonyesha wito wa kuachana na nishati ya mafuta kiskuku umepewa kisogo, na kusababisha kilio kutoka kwa nchi zilizo katika mazingira magumu ya mabadiliko ya tabianchi na mashirika ya kiraia..
  2. Huko Gaza hali ya kibinadamu inazidi kudororora huku mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakipaza sauti ya kunusuru maisha ya watu wanaopitia adhabu ya jehanamu duniani. Lile la afya WHO linataka ulinzi na fursa ya kufikisha huduma za kibinadamu, wakati la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA likisema karibu Gaza nzima inazingirwa na kusababisha adhabu ya pamoja kwa zaidi ya watu milioni 2 ambapo nusu yake ni watoto. 
  3. Na leo ni siku ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba maudhui “Afya kwa wote, wakati wa kuchukua hatua” Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO Dkt. Tedross Ghebreyesus katika ujumbe wake wa siku hii amesema “Huduma za afya kwa wote inamaanisha kwamba watu wote wanaweza kupata huduma wanazohitaji bila gharama kubwa lakini bado nusu ya watu wote duniani hawana huduma muhimu za afya. WHO ilizaliwa miaka 75 iliyopita kwa Imani kwamba afya ni haki ya binadamu na njia bora ya kutimiza haki hiyo ni huduma za afya kwa wote. 
  4. Mashinani tutaelekea nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyosaidia wafugaji kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'10"