Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 DESEMBA 2023

11 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na wakulima nchini Sudan kusini. Makala tunamulika madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watototo na mashinani tunakupeleka nchini DRC kwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu. 

  1. Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ukifikia ukingoni huko Dubai, Falme za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka washiriki waepuke msemo wa “Funika kombe mwanaharamu apite,” na badala yake waje na majawabu ya kina na ya kijasiri ili lengo la kutozidi kwa nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi liweze kufikiwa.
  2. Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukijiandaa kufunga pazia hapo kesho nakupeleka Sudan Kusini jimbo la Equatorial Mashariki ambako wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi sasa wanajengewa mnepo na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na wengi wameweza kujikwamua pamoja na familia zao. 
  3. Katika makala wakati pazia la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 likitarajiwa kufungwa hapo kesho huko Dubai Falme za kiarabu tunaangazia suala la jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watoto hususani katika suala la Afya na kwenye elimu. 
  4. Na mashinani tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC kwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu.  

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'10"