Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

01 DESEMBA 2023

01 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia siku ya UKIMWI duniani na Mkutano wa COP28.  Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?

  1. Leo ni siku ya UKIMWI duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030  huku Afrika, Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. 
  2. Na sasa tuangazie majanga ya asili. Mkutano wa COP28 ukiendelea Dubai, Falme za kiarabu kusaka suluhu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huko Somalia mafurikio makubwa yameendelea kusababisha zahma kwa wananchi ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA umezungumzia hali halisi na nini kinafanyika.
  3. Makala inatupeleka mkoani Shinyanga nchini Tanzania ambako huko mtandao wa kitaifa wa maendeleo ya afya, huduma na uegemezi wa watu waishio na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, SHDEPHA+, unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Ukimwi duniani, Jamii iongoze katika harakati za kutokomeza Ukimwi.
  4. Katika mashinani utasikia ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabili Ukimwi UNAIDS

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'51"