Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za Posta zisienguliwe kwenye uwekezaji – UPU

Huduma za Posta zisienguliwe kwenye uwekezaji – UPU

Pakua

Uwekezaji kwenye huduma za posta hasa katika nchi zinazoendelea kama zile za barani Afrika husalia nyuma kutokana na huduma hiyo kutopatiwa kipaumbele sana katikati ya changamoto kama vile afya, elimu, chakula, mabadiliko ya tabianchi. 

Hali hiyo husababisha huduma za posta kukosa ufadhili unaotakiwa, amesema Mutua Muthusi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la posta duniani, UPU katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Bwana Muthusi anasema mizani ya huduma zinazohitajika kwa njia moja au nyingine huacha posta nyuma, licha ya kwamba huduma hiyo ilionekana umuhimu wake wakati wa janga la coronavirus">COVID-19. Je ni kwa vipi, na nini kifanyike kuhakikisha uwekezaji unakuwa wa kutosha na posta ichangie kwenye maendeleo endelevu zama za sasa za maendeleo ya kidijitali? Bwana Muthusi anaanza kwa kuelezea changamoto zinazokumba huduma za posta katika nchi zinazoendelea. 

 

(H4) NB: Mahojiano haya yamefanikishwa na Kayla Redstone wa UPU. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'23"
Photo Credit
UPU