Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 OKTOBA 2023

17 OKTOBA 2023

Pakua

Hii leo jaridanitunakuletea mada kwa kina na ukulima wa kisasa hususani mijini umeelezwa kuchangia si tu upatikanaji wa chakula bali pia unatumia maji kidogo hivyo unapigiwa chepuo hususan wakati huu dunia ikikabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Taasisi ya Malembo Farm iliyofanya kazi nchini Tanzania na Kenya inatoa mafunzo ya kilimo cha kisasa mijini ambapo tumezungumza na wanufaika wa mafunzo hayo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wake Lucas Elias Malembo akiwa nchini Tanzania anayeanza kwa kueleza namna wanavyoienzi kauli mbiu ya mwaka huu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani, zinahusu nini? Salía papo hapo tafadhali!

  1. Asante Leah naazia Mashariki ya Kati ambako mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine yameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hatma raia huko Gaza na Ukingo wa Magaribi yakisistiza fursa ya kufikisha misaada kwa wenye uhitaji likiwemo shirika la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linalohifadhi wakimbizi wa ndani takribani 400,000 kati ya laki sita sasa katika vituo vyake.
  2. Katika taarifa nyingine leo UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limetoa tahadhari kuhusu kukithiri kwa ghasia na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika majimbo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambazo zimesababisha wimbi jipya la watu kukimbia makazi yao, ndani na nje ya nchi. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, UNHCR imeripoti kuwa zaidi ya watu 90,000 katika maeneo ya Rutshuru na Masisi wamelazimika kukimbia makazi yao katika wiki za kwanza za Oktoba. 
  3. Nchini Sudan kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Takriban watu 4,000 wameuawa huku mali na miundombinu ya raia      vikiharibiwa vibaya katika vita inavyoendelea Darfur na watu wengine 8,400 wamejeruhiwa, kati ya Aprili 15 na mwisho wa Agosti, huku wengi wao wakilengwa kutokana na sababu za kikabila, hasa eneo la Darfur Magharibi.
  4. Na mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina kushuhudia jinsi ambavyo watoto na jamii zao wanavyoathirika kufuatia vita kati ya Hamas na Israeli.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'6"