UPU na harakati za kusaidia nchini kusongesha posta za kidijitali
Leo ni siku ya posta duniani ambapo maudhui ni Pamoja kwa kuaminiana:Ushirikiano kwa mustakabali salama na uliounganika. Lengo la maudhui hay ani kuchagiza serikali na huduma zao za posta kusaidia maendeleo ya posta ya kidijitali ambayo itaboresha mtandao wa kale wa posta ulioendelezwa karne na karne, ukihitaji kwa kiasi kikubwa mtoa huduma na mhudumiwa kuonana uso kwa uso, jambo ambalo sasa kwa kiasi kikubwa limebadilika, huduma za posta mtandao zikichukua fursa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU linataka ofisi za posta zichochee uchumi wa kidijitali.
Katika kufahamu UPU inafanya nini kusongesha hilo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika hilo, Mutua Muthusi anazungumza na Evarist Mapesa wa Idhaa hii na anaanza kwa kuelezea hali ya huduma ya posta hususan katika nchi zinazoendelea au maskini katika zama za sasa za maendeleo ya kidijitali. Mahojiano haya yamefanikishwa na Kayla Redstone wa UPU.