09 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Mashariki ya Kati, Ulaya, siku ya posta duniani na mashinani anaelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumsikia mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.
1. Mapigano huko Mashariki ya Kati yakiingia siku ya tatu kati ya Israel na wapalestina, huko Geneva, hii leo wajumbe wa mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka mamia ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kurusha makombora kuelekea upande wa Israel.
2. Ili kuhakikisha mahitaji ya muda mfupi, kati na ya muda mrefu yanatimizwa, mashirika ya kibinadamu yanaendelea kuhaha kutafuta ufadhili wa haraka ili kuongeza msaada kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 nchini Armenia waliokimbia eneo la Karabhak kufuatia kuongezeka kwa uhasama mwezi Septemba.
3. Makala ni siku ya Posta Duniani ambapo Evarist Mapesa wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU Mutua Muthusi anaelezea nafasi ya maendeleo ya kidijitali katika kusongesha huduma za posta.
4. Mashinani ni mnufaika wa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP nchini DR Congo.