Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 OKTOBA 2023

03 OKTOBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na inatupeleka Kibokoni, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya ambako mabwawa ya samaki yamebadili kabisa maisha ya wavuvi wa eneo hilo walioathirika na mabadiliko ya tabianchi yaliyosabisha samaki kutoweka baharini na kuwakatisha tamaa ya Maisha. Lakini sasa kupitia mradi wa ufugaji samaki ulio chini ya mwamvuli wa Umoja Self-Help Group jamii hiyo ina mabwawa 17 ya samaki yanayozalisha samaki aina ya milkfish, kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na perege au tilapia. Mshiani tanakuletea ujumbe kusu afya ya uzazi na uswa wa kijinsia. 

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo limeonya kwamba hali ya njaa inaibuka kwenye mpaka kati ya Sudan Kusini na Sudan huku familia zinazokimbia mapigano nchini Sudan zikiendelea kuvuka mpaka kila siku. Takwimu mpya zilizokusanywa na WFP zinaonesha kuwa kati ya karibu watu 300,000 ambao wamewasili Sudan Kusini katika miezi mitano iliyopita, mtoto mmoja kati ya watano ana utapiamlo na asilimia 90 ya familia wanasema wanakaa siku nyingi bila kula.
  2. Leo imetimia miaka 10 kamili tangu ajali ya meli iliyokuwa imebeba wahamiaji zaidi ya 500 kutoka Libya barani Afrika kuelekea nchini Italia ilipozama kwenye eneo la Lampedusa.  Katika taarifa ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, Amy E. Pope, na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,(UNHCR) Filippo Grandi wamesema tukio hilo baya lilipotokea dunia iliahidi, “isitokee tena” lakini hilo halijatekelezeka.  Mwaka huu pekee kufikia jana Oktoba pili tayari watu 2,517 wameshahesabiwa kuwa wamefariki dunia au kupotea katika bahari ya Mediterania.
  3. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema leo kuwa Armenia inakabiliwa na changamoto za kiafya kutokana na wimbi la wakimbizi ambalo halijawahi kushuhudiwa. Lakini wakati huo huo mashirika ya Umoja wa Mataifa kama la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu duniani UNFPA limepeleka vifaa vya afya ya uzazi na la Kuhudumia Watoto UNICEF limeanzisha eneo salama huko Goris, kusini mwa Armenia.
  4. Katika mashinani Dk. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA anatoa ujumbe kuhusu upatikanaji wa afya Uzazi kwa wote, na usawa wa kijinsia.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'35"