Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MINUSCA kwa TANBAT6 - Zingatieni uhusiano mwema na raia

Mkuu wa MINUSCA kwa TANBAT6 - Zingatieni uhusiano mwema na raia

Pakua

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Jenerali Humphrey Nyone amewataka walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu nchini humo chini ya MINUSCA kuendelea na moyo wa uchapa kazi huku wakizingatia kuepuka unyanyasaji na unyonyaji wa kingono. 

Akitokea katika makao makuu ya MINUSCA yaliyoko kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui (tamka Bongii) takribani kilometa 292 magharibi mwa Mambéré-Kadéï, Jenerali Humphray Nyone ametua katika uwanja wa ndege wa mjini wa Berberati na baadaye akiambatana na wanadhimu wa kijeshi akazungumza na askari wa Kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT6 wanaohudumu chini ya MINUSCA, 

"Askari mila na desturi yake ni nidhamu na kufuata maelekezo. Hapa mlipo nimempata taarifa kutoka kwa kamanda Kikosi hiki Luteni Kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani jinsi mnavyo jituma katika utendaji kazi wenu nimefurahi sana kusikia hivyo. Aidha hii ni kweli kwamba kikosi hiki kinasaidia kikundi changu vyema katika kutekeleza na kukamilisha jukumu la MINUSCA hapa Jamhuri ya Afrika ya Kati ninawasihi kuendelea hivyo bila kusahau kuzidi kuepuka suala zima la unyanyasaji wa kingono. Asante sana."

Naye Kamanda wa TABAT6 Luteni Kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani amesema amepokea na kuahidi kudumisha aliyoelekezwa katika katika utendaji wa kikosi hicho cha walinda amani kutoka Tanzania.

Audio Credit
Kapteni Mwijage Inyoma
Audio Duration
1'49"
Photo Credit
TANBAT6/Kapteni Mwijage Iyoma