28 AGOSTI 2023
Pakua
Hii leo jaridani jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Zimbabwe baada ya uchaguzi na masuala ya afya nchini Botswana. Makala tunakupeleka nchini Mali na mashinani nchini Rwanda, kulikoni?
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anafuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye mchakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe tarehe 23 mwezi huu wa Agosti
- Mkutano wa Sabini na tatu wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) umeanza hii leo katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone huku tukio hilo likishuhudia pia Maabara ya Kitaifa ya Marejeleo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ya Botswana ikipewa hadhi ya kuwa Kituo Kishiriki cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kufuatilia Ubora.
- Katika makala Assumpta Massoi anamulika harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA kuwa umeondoka nchini humo ifikapo tarehe 31 mwezi Desemba mwaka huu kufuatia ombi la mamlaka nchini Mali.
- Mashinani tunakupeleka nchini Rwanda kusikia ni kwa jinsi gani wazazi wameweza kutokomeza udumavu na kuhakikisha afya njema kwa watoto wao.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'12"