Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 AGOSTI 2023

25 AGOSTI 2023

Pakua

Hii leo jaridani jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Sudan na utaifa wa Wapemba nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Pakistan na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Vita inayoendelea nchini Sudan inachochea dharura kubwa ya kibinadamu ambapo vita na njaa, magonjwa na watu kufurushwa makwao vilivyofuatia sasa inatishia ‘kutafuna’ nchi nzima, amesema Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Martin Griffiths
  2. Mwishoni mwa mwezi uliopita Rais wa Kenya William Ruto akiwa Kilifi mashariki mwa Kenya alitangaza kutambulika rasmi kwa jamii ya Wapemba ambao kwa miaka mingi waliishi nchini humo wakikosa hadhi ya utaifa kwa kuwa vizazi vyao vya nyuma vilitoka nje ya Kenya. 
  3. Makala tunakwenda Pakistani ambako leo ni mwaka mmoja tangu mafuriko makubwa yaliyozua zahma nchini humo.
  4. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kushuhudia jinsi ambavyo ukulima wa mboga mboga  na matunda unavyosaidia wanawake kupatia jamii zao mapato thabiti na kuwapeleka watoto wao shuleni.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
9'56"