Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 AGOSTI 2023

22 AGOSTI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Mapigano yanayoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yakiendeshwa na vikundi vilivyojihami vya waasi yanaendelea kufurusha watu kutoka makwao, na hivyo wakimbizi hao wa ndani kushindwa kujikimu maisha yao ya kila siku. Malazi ni shida, makazi ni shida, halikadhalika chakula. Maisha yanakuwa ni changamoto kila uchao. Hali hiyo iko dhahiri kabisa jimboni Kivu Kaskazini ambako hata hivyo hatua za shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP kwa wakimbizi Oicha zimeleta ahueni. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za msaada wa kibinadumu, malaria na maji. Mashinani tunakwenda Tanzania hususan mkoani Kilimanjaro.

  1. Mamilioni ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wako hatarini kukumbwa na njaa huku ufadhili ukiwa katika hali mbali ametahadharisha leo Peter Musoko ambaye ni Mkurugenzi wa Nchi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) nchini DRC alipozungumza leo na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi. 
  2. Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi amehutubia mkutano wa Wiki ya Maji huko Stockholm nchini Sweden na kutaka mabadiliko makubwa ya hatua za kufanikisha upatikanaji wa maji duniani akisema kwa kasi ya sasa muda uliosalia hautawezesha kufanikisha lengo la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu maji.
  3. Na Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) umetangaza Mbinu Mpya ya Kuongeza Upatikanaji wa Vyandarua Vizuri Zaidi ili Kuzuia Malaria. 
  4. Na mashinai Anna Assey, mkulima kutoka mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania akielezea ni kwa vipi yeye anahifadhi mbegu za kiasili wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasisitiza matumizi ya mbinu za kiasili kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'59"