21 AGOSTI 2023
Pakua
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya waathirika wa ugaidi duniani na mabomu ya kutegwa ardhini. Makala tunakupeleka nchini Siarra Leone na mashinani nchini Msumbiji, kulikoni?
- Ikiwa leo tarehe 21 Agosti ni Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Waathirika wa Ugaidi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii amewasihi watu wote ulimwenguni kuhakikisha kwamba wale waliofariki au kukumbwa na athari za muda mrefu za ugaidi hawasahauliki kamwe.
- Huko nchini Lebanon, Mashariki ya Kati, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIFIL kwa ushirikiano na wadau wameteketeza mabomu 4,000 yaliyokuwa yametegwa kwenye eneo la ukubwa wa mita 44,000 za mraba na hivyo kuwezesha ianze kutumika tena kwa kilimo baada ya kushindikana tangu miaka ya 1970 kwa hofu ya milipuko ya mabomu.
- Katika makala Leah Mushu anatujuza namna nchi ya Sierra Leone ilivyoweza kubadilika kutoka nchi yenye ugunduzi dhaifu wa magonjwa hususan ya mlipuko mpaka kuwa nchi yenye ugunduzi thabiti na unaofanya kazi.
- Mashinai tunakwenda mjini Maputo nchini Msumbiji kusikia jinsi huduma ya maji ilivyoleta furaha kwa wafanyabiashara.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'56"