Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manusurua kutoka Gambia: Sitamani tena kuzamia kwenda ulaya

Manusurua kutoka Gambia: Sitamani tena kuzamia kwenda ulaya

Pakua

Kila mwaka maelfu ya wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika hujaribu kufika Ulaya wakivuka Bahari ya Mediterania wakieleza kwenda kusaka maisha bora lakini safari hiyo inaelezwa kuwa ni hatari sana kwani maelfu ya watu hufa maji au kutoweka. 

Ni Amadou Jobe kijana ambaye akiwa na umri wa miaka 25 alianza safari ya hatari kutoka nchini Kwake Gambia kupitia kaskazini mwa Afrika lengo likiwa Kwenda nchini Italia kusaka maisha bora kwani alikuwa akiishi katika hali ya umasikini na alitamani kuja kuisaidia familia yake iwapo angefanikiwa kufika Ulaya. 

Safari ya Amadou haikuwa rahisi kwa zaidi ya miaka miwili alikuwa safarini kutoka nchini mwake Gambia alienda mpaka nchi ya Mauritani, kisha Mali, akaingia Niger na mwisho nchini Libya nchi ambayo baada ya kukaa zaidi ya mwaka mmoja alifanikiwa kupata boti ambayo ndio ingetimiza ndoto yake ya Kwenda Ulaya. 

“Ndani ya boti yetu, kulikuwa na zaidi ya watu 100 kutoka Gambia, watu wengine niliowakuta ni Wanigeria na wengine wanatoka Liberia kiufupi kulikuwa na nchi  kutoka barani Afrika. Siku tulipojaribu kuvuka Kwenda Ulaya, boti yetu ilikuwa na matatizo na hali ya hewa pia haikuwa nzuri. Tuliona maji yakijaa ndani ya boti yetu. Kwa hivyo tuliamua kurudi kwa sababu kama tukitaka kuendelea, tungaweza wote kufamaji huko.” 

Bahati haikuwa yake kwani alipojaribu kusafiri awamu ya pili walikamatwa na kufingwa jela nchini Libya anasema maisha jela yalikuwa mabaya na baadae Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM liliwatembelea gerezani na kuwapa fursa ya kurejeshwa makwao na Amadou naye alirejea.

“Sikuwa nataka kurudi hapa. Nilitaka kuendelea na safari yangu. Nina huzuni sana kwa sababu pesa zote nilizotumia, nilipoteza kila kitu na kuja kuanza upya kutoka sifuri. Nimetumia karibu dola 1700. Lakini hakuna la kufanya. Mahali tulipokuwa tusingeweza kwenda kokote na hauwezi kutoroka.” 

Marie Stella Ndiaye ni meneja program wa IOM nchini Gambia anaeleza baada ya kuwajeresha makwao hawawaachi pia wa programu za kuwasaidia.  

“Tumejikita kwenye kuwatafuta na kuokOa maisha yao. Pia tunatoa usaidizi kwenye vituo vya rasilimali za wahamiaji vilivyo katika nchi ambazo wahamiaji hawa hupita wakitaka kusafiri Kwenda ulaya. Mara tu wanaporejea, IOM inatoa usaizi wa kila aina kuanzia masuala ya ushauri nasaha, ujumuishaji wa kiuchumi, ujumuishaji upya wa kijamii, lakini pia, muhimu zaidi, usaidizi wa kisaikolojia.” 

Mara bada ya kurejea nchini Gambia Amadou alipata ufundi stadi kutoka mashirika ya UN ambayo ni IOM na UNCDF na sasa anafanya kazi ya fundi uashi, ameoa na ana watoto wawili. Ameapa kutojaribu tena kuzamia kwenda ulaya, ataenda bara hilo kwa kupanda ndege kihalali nasi vinginevyo.  

Audio Credit
Evarist Mapesa
Audio Duration
3'19"
Photo Credit
UN News/ Hisae Kawamori