11 AGOSTI 2023
Pakua
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Vijana Duniani ambayo inaadhimishwa tarehe 12 Agosti 2023 kila mwaka na tutafuatilia kazi za vijana waliorejea nyumbani Gambia kutoka Ulaya. Pia tuanaangazia msaada wa kibinadamu Sudan. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, salía papo hapo!
- Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hatimaye limethibisha hofu yake juu ya viwango vya juu vya njaa nchini Sudan baada ya kuweza kwa mara ya kwanza kufikisha msaada wa chakula kwa wakazi wa Darfur Magharibi nchini humo tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili mwaka huu huku mamilioni ya watu wakiwa hawana chakula. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
- Kila mwaka maelfu ya wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika hujaribu kufika Ulaya wakivuka Bahari ya Mediterania wakieleza kwenda kusaka maisha bora lakini safari hiyo inaelezwa kuwa ni hatari sana kwani maelfu ya watu hufa maji au kutoweka. Evarist Mapesa anatupeleka nchini Gambia kusikia simulizi wa kijana ambaye chupuchupu apoteze maisha.
- Hii leo katika Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mwandishi wetu George Musubao amezungumza na kijana Florent Muhindo Nambura mkazi wa Beni jimboni Kivu Kaskazini ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya vijana duniani tarehe 12 mwezi huu wa Agosti. Florent anaanza kwa kuelezea kile afanyacho.
- Mashinai tunakupeleka katika kambi ya wakimbizi ya Birau nchini CAR, ambako kijana mkimbizi kutoka Sudan hajafa moyo na anatarajia kutimiza ndoto zake na zile za watoto wakibizi walioko kambini humo.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'10"