Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 AGOSTI 2023

04 AGOSTI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu na Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’.  Makala tunakupeleka nchini Brazil na mashinani tutasikia ujumbe wa kijana kutoka Tanzania, salía papo hapo!  

  1. Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu UN Volker Türk, hii leo ameelezea masikitiko yake makubwa kufuatia kufungwa kwa ofisi yake nchini Uganda kufuatia uamuzi wa serikali hiyo kutotia saini mkataba wa kuendelea kuweko kwa ofisi hiyo nchini humo. 
  2. Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametimiza ahadi yake ya kuunda Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi wakati huu ambapo teknolojia ya Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’ imeshaanza kugonganisha vichwa vya watu kuhusu nafasi yake katika maendeleo duniani.
  3. Katika makala Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ziarani nchini Brazil amewahakikishia watu wa jamii ya asili ya Mapuera kwenye jimbo la Pará nchini humo kwamba amesikia kilio chao na zaidi ya yote Umoja wa Mataifa utahakikisha sauti zao zinasikilizwa kwani wanachodai ni haki zao za msingi.
  4. Na katika mashinani na ikiwa tunaelekea siku ya vijana duniani nampisha tutasikia ujumbe wa kijana Najma Mohamed kutoka Tanzania ambaye ni bingwa wa haki za watoto kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia watoto UNICEF.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
11'25"