Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 JUNI 2023

27 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo inaturejesha hapa Makao makuu ya umoja wa Mataifa kusiki maandalizi ya maadhimisho ya pili ya siku ya Lugha ya Kiswahili duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu watoto katika migogoro ya silaha, msaada kwa wakimbizi nchini Sudan na maadili ya akili bandia. Katika mashinani tunakupeleka nchini Mali, kulikoni?

  1. Ikiwa leo ni Siku ya Biashara Ndogondogo na za Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapigia chepuo wanawake na wajasiriamali wadogo kwamba wanahitaji kusaidiwa ili kukabiliana na changamoto nyingi ambazo mara nyingi huzuia ukuaji wa biashara zao, na kuwakwamisha wengi wao katika ujasiriamali usio rasmi.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeeleza kuwa linazidi kutishwa na kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu miongoni mwa walioathirika na vita nchini Sudan. Kamishna Mkuu Msaidizi wa Operesheni za UNHCR, Raouf Mazou hii leo mjini Geniva Uswisi amesema wafanyakazi wa UNHCR wanafanya juhudi za kusaidia wananchi lakini ukosefu wa usalama unazuia kufika katika baadhi ya maeneo ili kuwasaidia wenye uhitaji.   
  3. Na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Kamisheni ya Ulaya wametia saini makubaliano ya kuharakisha utekelezaji wa kimataifa wa Pendekezo la UNESCO kuhusu maadili ya akili bandia. Bajeti ya Euro milioni 4 itatolewa kusaidia nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani ili zifanikishe uundaji wa sheria zao za kitaifa. Takriban nchi 30 tayari zimeanza kutumia Pendekezo hili kutunga sheria za kitaifa zinazohakikisha kwamba matumizi ya akili bandia yanaheshimu uhuru wa kimsingi na haki za binadamu na kuwanufaisha wanadamu wote.
  4. Mashinani tutakupeleka nchini Mali ambapo tutaskikiliza jinsi vita inavyoathiri watoto.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
15'49"