Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 MEI 2023

30 MEI 2023

Pakua

Jaridani hii leo ni mada kwa kina leo tunaelekea nchini DRC kuangazia kikosi cha pili cha walinda amani kutoka Kenya cha kuchukua hatua za haraka KEN QRF 2 kinachohudumu mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, DRC-MONUSCO. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo  za matumaini kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo nchini Sudan, msaada wa kibinadamu kwa watoto nchini humo, na wakimbizi wanaohama kwa nchi jirani. Mashinani tutakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo Jumanne limeeleza kuwa kwa mara ya kwanza tangu mapigano yazuke nchini Sudan tarehe 15 Aprili, wahudumu wa kibinadamu sasa wameweza kufikisha msaada wa chakula kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo huo, Khartoum.    
  2. Tukisalia na taarifa kuhusu hali ya Sudan, hii leo pia Msemaji wa UNICEF James Elder amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba "watoto wengi zaidi nchini Sudan wanahitaji usaidizi wa kuokoa maisha kuliko hapo awali", huku watoto milioni 13.6 wakihitaji msaada wa haraka. Na akifanya kulinganisha idadi hiyo  akasema kwamba, "Hii ni zaidi ya idadi ya watu wote wa Sweden, Ureno au Rwanda,"
  3. Na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Misri ametoa wito wa dharura wa msaada kwa watu wanaokimbia Sudan na akazisihi nchi zinazowapokea wakimbizi wa Sudan kuendelea kuacha mipaka yao wazi kwa ajili ya wale wanaotoroka vita.
  4. Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Kamishna Suzan Kaganda ambaye anahusika na Utawala na Raslimali watu katika Jeshi la Polisi Tanzania akizungumzia mikakati ya Jeshi la Polisi la Tanzania kushiriki katika shughuli za ulinzi wa amani duniani.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
12'5"