Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 MEI 2023

26 MEI 2023

Pakua

Jaridani hii leo tunaangazia ripoti kuhusu matumizi ya tumbaku na wakimbizi wa Sudan. Makala tunaangazia mauaji ya kimbari nchini Rwanda na mashinani tutakupeleka nchini Chad, kulikoni?

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezisihi nchi kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na badala yake kuelekeza usaidizi wao kwenye mazao endelevu yatakayo wanufaisha mamilioni ya watu. 
  2. Walimuua mume wangu, walijeruhi mwanangu na mimi walinipiga, ni simulizi ya mama ambaye sasa yuko na watoto wake nchini Chad akitokea Sudan kwani nchini mwake ni kama wasemavyo wahenga, Amkani si shwari kufuatia mapigano yaliyoanza tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu ambayo pamoja na kuua zaidi ya watu 700 wengine zaidi ya 300,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Chad na miongoni mwao ni Hawaye Ibrahim.
  3. Makala Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania,  Serge Brammertz ameeleza ni kwa nini ilichukua muda mrefu wa zaidi ya miaka 20 kumtia mbaroni Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei 24 huko Paarl nchini Afrika Kusini na leo kufikishwa katika mahakama ya Afrika Kusini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumrejesha nchini Rwanda ili akabiliane na mkono wa sheria.
  4. Katika mashinani na tukiwa tunaelekea siku ya walinda amani duniani leo tutaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR kusikiliza ujumbe kutoka kwa mlinda amani akilezea umuhimu wa siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
14'21"