Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 MEI 2023

19 MEI 2023

Pakua

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akianzia barani Afrika, kisha Amerika ya Kusini na kurejea tena Afrika na kutamatishia barani Asia.

1. Nchini Malawi Umoja wa Mataifa waomba fedha zaidi kunusuru watoto dhidi ya udumavu na unyafuzi kutokana na changamoto lukuki kama vile magonjwa ya milipuko, madhara ya tabianchi na ufadhili duni kwenye sekta za kijamii.

2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) linaongeza juhudi za msaada wa kibinadamu kwenye mipaka ya Colombia, Costa Rica na Panama ili kusaidia wahamiaji wanaovuka kuelekea eneo la kaskazini mwa Amerika hasa kupitia msitu hatari wa Darien unaounganisha Amerika kusini na kaskazini. 

3. Makala anakurejesha Afrika mpakani mwa Sudan na Chad kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wanaokimbia mapigano Sudan wakiwemo maelfu ya watoto.

4. Mashinani anakupeleka nchini Sri Lanka kusikia ujumbe kuhusu ukulima wa chai na njia za kuipanda upya ili ilete mapato mazuri, ikiwa ni kuelekea siku ya chai duniani.

Audio Credit
ANOLD KAYANDA
Audio Duration
14'12"