Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 MEI 2023

17 MEI 2023

Pakua

Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na mchakato wa uchaguzi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani yunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani.

  1. Mzozo nchini Sudan ukiingia mwezi wa pili, hii leo Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanyia marekebisho ombi la usaidizi kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu wengine waliokimbilia nchi jirani kusaka usalama. 
  2. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefanya warsha za majadiliano katika mji wa Torit na Magwi mashariki mwa mji mkuu Juba jimboni Equatorial Mashariki ili kujadili kuhusu utungaji katiba na michakato ya uchaguzi.
  3. Makala leo inatupeleka Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linashirikiana na serikali na wadau wengine kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya na malezi bora ijulikanayo kama NICHE.
  4. Katika mashinani tutasikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani na jinsi ambavyo inatofoutiana kulingana na nchi.

Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda