09 MEI 2023
Pakua
Jaridani hii leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika jitihada za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendeleza lugha ya Kiswahili kimataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo machafuko nchini Sudan, uzazi salama na masuala ya afya . Mashinani tunakupeleka nchini Ethiopia.
- Idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan waliotawanywa na machafuko mapya ynayoendelea imeongezeka zaidi ya mara mbili wiki iliyopita na sasa kufikia watu 700,000 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, leo limezindua ripoti mpya inayoelezea hatua zilizopigwa kuhusu kuokoa maisha wakati wa kujifungua, na vifo vya watoto wachanga.
- Katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Baraza kuu kunafanyika mkutano wa siku mbili wa ulioandaliwa kwa pamoja na Baraza Kuu la umoja wa Mataifa na WHO, ukiwaleta pamoja wadau mbalimbai kuzungumzia masuala muhimu ya afya ikiwemo na huduma za afya kwa wote.
- Mashinani tutaelekea Tigray nchini Ethiopia kushuhudia kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua na harakati za kusaidia watoto ambao wako hatarini kuathirika na utapiamlo.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
11'29"