Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 APRILI 2023

27 APRILI 2023

Pakua

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika harakati za kufanikisha kilimo hifadhi nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya UNICEFya wasichanan katika ICT, watoto katika mizozo nchini Sudan na chanjo kwa watoto katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Na katika jifunze Kiswahili hii leo tuko Tanzania kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno"NDUI".

  1. Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya wasichana katika TEHAMA,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema asilimia 90 ya wasichana vijana na barubaru hawatumii mtandao wa intaneti hasa katika nchi za kipato cha chini wakati wenzao wa kiume wana fursa karibu mara mbili ya kuwa mtandaoni, ndio maana maudhui ya mwaka huu ya siku hii ni “Ujuzi wa kidijitali kwa Maisha” ili kuchagiza wasichana na wanawake kushamiri katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati au STEM.
  2. Wakati makubaliano ya usitishaji uhasama yakikaribishwa nchini Sudan, mashirika ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa yameendelea kuonya kuhusu hatari inayowakabili watoto na kuathirika kwa mfumo wa afya. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, taasisi iliyo ya kiserikali ya Worls Vision na Save the children wameelezea jinsi gani watoto walivyo katika hatari kubwa endapo muafaka huo wa kusitisha uhasama hautotekelezwa na kuheshimiwa na pande zote, huku shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO likionya kuhusu kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya afya ikiwemo kukaliwa na wapiganaji hospital kadhaa mjini Kharthoum pamoja na maabara kuu.
  3. Na zaidi ya watoto milioni 4.3 katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MENA) hawajapokea hata chanjo moja ya surua kati ya mwaka 2019 hadi 2021 limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kuongeza kwamba watoto wengine takriban milioni 3.8 walipata chanjo pungufu za donda koo, pepo punda na pertussis(DTP) katika kipindi hicho.
  4. Na katika jifunze Kiswahili leo tuko Tanzania kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno"NDUI".

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'16"