Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 APRILI 2023

06 APRILI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunaangazia afya ya uzazi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya afya ya uzazi salama kwa wanawake kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dk. Elieza Chibwe akizungumzia juu ya kukoma kwa hedhi kwa wanawake anasema “Ukihisi dalili za menopause mapema nenda hospitali.” Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo salamu za sikukuu za Pasaka na Eid El Fitr kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ombi la UNICEF la msaada kwa watoto waathirika wa matetemeko ya ardhi huko mashariki ya kati, na haki za watu wa jamii asili. Leo katika kujifunza kiswahili Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya uchambuzi wa methali isemayo “Mshale kwenda msituni haukupotea.”

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa watu wa imani zote duniani kote "kuunganisha sauti zao katika maombi ya pamoja ya amani", wakati huu dunia ikijiandaa kusherehekea sikukuu za Pasaka na Eid El Fitr huku akikiri kwamba amani imekosekana.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limesema miezi miwili baada ya metetemeko ya ardhi yaliyopiga Uturuki na kaskazini mwa Syria, bado watoto milioni 2.5 nchini Uturuki wanahitaji msaada na wako hatarini kutumbukia kwenye umaskini, kutumikishwa kwenye ajira au kuozwa utotoni.
  3. Na mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa jamii ya asili hii leo amekaribisha hatua ya Vatican kutupilia mbali Nyaraka ya Ugunduzi, ambayo ni amri ya Kanisa Katoliki ya Zaidi ya miaka 500 iliyotumika kuhalalisha wakoloni kutwaa ardhi ya watu wa jamii ya asili.
  4. Na katika kujifunza kiswahili mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale kwenda msituni haukupotea.”.

Mwenyeji wako Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'2"