Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 APRILI 2023

04 APRILI 2023

Pakua

Hii leo ni siku ya mada kwa kina ambapo leo tutasafiri pamoja hadi visiwani Zanzibar nchini Tanzania kusikia harakati binafsi za mke wa Rais katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ili kusaidia wanawake, wasichana, vijana na watoto. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za afya uzazi , athari za mabomu ya ardhini na ubaguzi dhidi ya raia weusi nchini Tunisia. Mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu athari za mabomu ya ardhini.

  1. Idadi kubwa ya watu wameathiriwa na utasa kwenye maisha yao, imeeleza ripoti mpya iliyochapishwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO.
  2. Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji na usaidizi dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini maudhui yakisema “Hatua dhidi ya mabomu haiwezi kusubiri”. Katika ujumbe wake wa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwa mamilioni ya watu wanaoishi katika maeneo yenye migogoro ya silaha hata pale ambapo migogoro hiyo itamalizika bado maeneo yao yanasalia kutokuwa salaama.
  3. Na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inayopiga vita ubaguzi wa rangi CERD imeitaka mamlaka ya ngazi za juu nchini Tunisia kulaani hadharani na kujitenga na kauli za chuki na kibaguzi zinazotolewa na wanasiasa, watu mashuhuri na watu binafsi dhidi ya Waafrika weusi, hasa wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara na raia weusi wa Tunisia.
  4. Na mashinani tutakuletea ujumbe wa Danel Craig, Balozi Mwema wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya huduma za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini, UNMAS kuhusu athari za mabomu ya ardhini.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'54"