Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 APRILI 2023

03 APRILI 2023

Pakua

Jaridani leo tunaangazia mahitaji ya kibinadamu nchini Burundi, na uwekezaji wa elimu nchini Colombia. Makala tunaelekea tunaku[eleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia huko huko nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Wadai wa masuala ya kibinadamu kwa kushirikiana na serikali ya Burundi leo wamezindua ombi la pamoja wakihitaji dola milioni 194.2 kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya kibinadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2023.
  2. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza elimu kwenye maeneo ya mizozo, Education Cannot Wait, ECW, au Elimu Haiwezi Kusubiri umetangaza nia yake ya kupanua uwekezaji nchini Colombia kwa kuwekeza dola milioni 12 ili uweze kuwafikia watoto wengi zaidi raia wa Colombia na wakimbizi kutoka nchini Venezuela.
  3. Katika makala leo tunaanza mfululizo wa vipindi vitavyoendelea hadi tarehe 10 Desemba kilele cha siku ya haki za binadamu, mwaka huu ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa azimio la tamko la haki za binadamu. Tamko hilo lina ibara 30 na leo tunaanza na ibara ya kwanza. Kuchambua ibara hiyo Stella Vuzo afisa habari wa kitucho cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es slaam ameketi na mwanasheria au wakili Bahame Tom Nyanduga ambaye pia aliwahi kuwa mwakilishi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.
  4. Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia jinsi ambavyo programu iliyofanikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA imewasaidia watu wenye ulemavu.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
14'26"