Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 MACHI 2023

28 MACHI 2023

Pakua

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo tutamsikia Spika wa Bunge la Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka UNICEF, ILO na OHCHR.  Mashinani tunakupeleka  nchini Malawi.

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la  kuhudumia watoto duniani UNICEF limetoa ombi la dola milioni 171 ili liweze kusaidia watu milioni 28 wanaokabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu katika nchi 11 zilizoko Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la ajira ulimwenguni ILO limesema matetemeko yaliyozikumba nchi za Syria na Uturuki  mapema mwaka huu yamesababisha biashara nyingi kufungwa na kuharibika kwa kiasi kikubwa na  matokeo yake mamia kwa maelfu ya watu katika nchi hizo hawana ajira za kuwapatia kipato ili waweze kujikimu.
  3. Na kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu Volker Turk hii leo jijini Geneva nchini Uswisi ametoa ripoti ya kina inayoonesha mateso yanayoendelea ya waathirika wa kutoweshwa  na kutekwa nyara nchini Korea Kaskazini na kutaka wale wote wanaohusika wachukuliwe hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani ndani ya nchi au mahakama za kimataifa.
  4. Katika mashinani Shorai Nyambalo Ng'ambi afisa wa UNICEF akiwa amembeba mtoto katika kambi  ya Naotcha mjini Blantyre nchini Malawi inayohifadhi waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na kimbunga Freddy nchini Malawi akitoa wito wa usaidizi kwa shirika hilo kwani mahitaji ya watoto ni makubwa na wanakumbwa na kiwewe!

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'38"