Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 MACHI 2023

24 MACHI 2023

Pakua

Jaridani leo tunaangazia siku ya kifua kikuu duniani na tunaelekea nchini Kenya. Pia tunakuletea yaliyojiri makao makuu katika mkutano wa maji.  Makala tunakupeleka DRC na Mashinani tunarejea makao makuu, kulikoni?

  1. Leo ni siku ya kifua kikuu duniani maudhui yakiwa “ndio inawezekana kuitokomeza TB.” Takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2000 watu milioni 74 wamesalimika baada ya Kupona kifua kikuu na ni kwasababu ya harakati za ulimwengu za kupambana na ugonjwa huo hatari.
  2. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ukifikia tamati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huku moja ya mikakati ni kuhakikisha kunakuweko matumizi endelevu ya maji, mmoja wa washiriki kutoka Rwanda amezungumzia vile ambavyo teknolojia ya kusafisha maji taka ili yaweze kutumika tena na tena inaweza kuwa mkombozi kwenye eneo lao.
  3. Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akiwa Beni amekutana na muathirika wa kuuawa kwa wanafamilia lakini hadi sasa haki haijatendeka, ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupata ukweli kwa makosa ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utu kwa waathiriwa hao.
  4. Na katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Danielle Kamtie, Makamu wa Rais wa Bunge la Vijana Duniani katika Maswala ya Maji ambaye ni mmoja wa vijana wanaohudhuria mkutano wa maji hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'14"