Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 MACHI 2023

23 MACHI 2023

Pakua

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo Mkutano wa 67 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 umekunja jamvi baada ya kufanyika kwa takribani wiki mbili! Maudhui yalikuwa ni vipi teknolojia na uvumbuzi vinaweza kumkwamua mwanamke na msichana katika zama za kidijitalitunaangazia, na Getrude Dyabene, Afisa kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania atakueleza washiriki waliondoka na ujmbe gani.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi za afya, maji safi na salama na biashara. Katika jifunze Kiswahili leo tunataungana na mtaalam wetu ni Onni Sigalla kutoka BAKITA,Tanzania  salia papo hapo?

  1. Kuelekea siku ya Kifua Kikuu au TB duniani hapo kesho shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO hii leo limetangaza kupanua wigo wa mpango wa Mkurugenzi wa shirika hilo wa kusaidia mchakato wa ufuatiliaji wa ugonjwa huo ili kuutokomeza na kufanikisha afya kwa wote ifikapo mwaka 2030. Mpango huo uliokuwa wa 2018 hadi 2022 sasa umeongezwa kutoka 2023 hadi 2027 na unajumuisha utoaji wa tiba za muda mfupi mfupi dhidi ya TB yenye usugu wa dawa.
  2. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ukiendelea hapa Umoja wa Mataifa mmoja wa washiriki Mana Omar ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la kiraia la SASAL Kaunti ya Kajiado nchini Kenya amezungumzia changamoto za maji zinazokabili jamii yake ya wafugaji.
  3. Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara, UNCTAD imetoa ripoti yake hii leo inayoonesha ingawa ukuaji uchumi duniani ulidorora mwishoni mwa mwaka jana na kuwa hasi, mwanzoni mwa mwaka huo kuwa kiwango cha biashara kilivunja rekodi na kufikia thamani ya dola trilioni 32 na kichocheo kilikuwa uzalishaji wa bidhaa rafiki kwa mazingira.
  4. Na katika jifunze lugha ya Kiswahili , leo tunapata ufafanuszi wa neno "HAKIBIZA" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'33"