Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 MACHI 2022

22 MACHI 2022

Pakua

Jaridani leo tunaangazia mkutano wa maji hapa makao makuu na kusalia kwenye siku ya maji tukimulika upatikanaji wa maji nchini DRC. Makala na mashinani tutasalia huko huko DRC, kulikoni?

  1. Ikiwa leo ni siku ya maji duniani Umoja wa Mataifa  umetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti sasa iki kuhakikisa rasilimali hiyo adhimu inalindwa, kudhibitiwa ipasavyo na kupatikana kwa kila mtu.
  2. Hii leo ni siku ya maji duniani na ninakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mtoto Liesse mwenye umri wa miaka 17 amefuatilia upatikanaji wa maji safi ya kunywa kwenye eneo la Goma jimboni Kivu Kaskaizini baada ya kupatiwa mafunzo ya uandishi wa habari na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF na hatimaye taarifa yake kutangazwa na Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo.
  3. Makala tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye makabidhiano ya vikosi vya Tanzania vya kutoa usaidizi wa haraka kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO. Shuhuda wetu ni Luteni Abubakar Muna, Afisa Habari wa walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania.
  4. Na katika mashinani namleta kwako Ghislane, mama huyu wa familia mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC akizungumzia jinsi maji wanayoteka ziwa Kivu ni machafu na yanasababisha magonjwa kwa mtoto wale mdogo. Akisema madayareee akimaanisha kuhara. Anatoa wito watu wasitupe taka kwani ziwa ni chanzo cha samaki, chakula na usafiri

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'17"