Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 MACHI 2023

20 MACHI 2023

Pakua

Hii leo katika jarida tunamulika upatikanaji wa huduma za maji na za usafi, siku ya furaha, kongamano la kiswahili Zanzibar, Tanzania na changamoto za maji yatokanyo ziwa Kivu mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

  1. Wakati viongozi wa dunia wakijiandaa kuhudhuria mkutano wa kihistoria wa maji wa Umoja wa Mataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF llimetoa wito wa uwekezaji wa haraka katika huduma za maji, usafi na usafi wa mazingira (WASH) zilizo na mnepo ili kuwalinda watoto. 
  2. Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumi
  3. Anold Kayanda wa Idhaa hii  ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Fatma Hamad, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Michezo katika serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhusu Kongamano la Idhaa za Kiswahili lililofanyika visiwani humo.  
  4. Mashinani: Paschal, mtoto mwenye umri wa miaka 15 ambaye kila siku kabla ya kwenda shule anadamkia Ziwa Kivu jimboni Kivu Kaskazini nchini DR Congo kuokota taka ili kuhakikisha wanaoteka maji hawapati magonjwa.
Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'3"