Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 MACHI 2023

16 MACHI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunanasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikiliza mahojiano yetu na viongozi waandamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto huko Zanzibar Tanzania wanaoshiriki mkutano wa 67 wa hali ya wanawake duniani, CSW67 maudhui yakiwa matumizi ya dijitajitali katika zama za sasa za teknolojia kwa lengo la kusaidia wanawake na wasichana na hatimaye jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo hali nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kuzuka nchini humo, Wakimbizi Ethiopia WHO na teknolojia UNCTAD. Katika kjifunza Klugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote, baki nasi!

  1. Nchini Malawi, Umoja wa Mataifa umeendelea kuchukua hatua za usaidizi baada ya Rais wa nchi hiyo Lazarus Chikwera kutangaza hali  ya hatari kwenye mkoa wa kusini kufuatia mvua kubwa zilizosababishwa na kimbunga Freddy na katika wiki hii pekee zaidi ya watu 170 wamekufa na 178 wameokolewa.
  2. Nchini Ethiopia, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linaimarisha harakati zake za kuhakikisha wakimbizi wanaokimbia ghasia Somalia na kuingia ukanda wa Dollo ulioko mkoa wa Somali nchini Ethiopia wanapata huduma za afya pamoja na wenyeji wao, wakati huu ambapo idadi yao inaongezeka kila uchao kwani tangu mwezi Februari mwaka huu idadi ya wakimbizi walioingia imefikia takribani laki moja.
  3. Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD imesema teknolojia rafiki kwa mazingira ambazo zinatumika kuzalisha bidhaa na huduma zinazidi kushamiri kila uchao na kuongeza fursa za kiuchumi, lakini nchi zinazoendelea ziko hatarini kutonufaika nazo iwapo serikali na jamii ya kimataifa hazitachukua hatua madhubuti.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na tunasalia visiwani Zanzibar nchini Tanzania ambako mchambuzi wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote..

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'23"