Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 MACHI 2023

15 MACHI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea tunaangazia vurugu nchini Syria ambapo ni miaka 12 kamili tangu machafuko yalipozuka; na ripoti ya ILO inayosihi nchi zote duniani ziboreshe mazingira ya kazi ya watendaji hao. Makala tutaelekea nchini Bahrain na mashinani nchini Geneva, kulikoni?.

  1. Leo ni miaka 12 kamili tangu machafuko yalipozuka Syria na kusababisha vita inayoendelea tangu mwaka 2011 iliyosambaratisha nchi hiyo na mamilioni ya raia wake. Maelfu wamepoteza maisha, mamilioni wamekuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao na majanga mengine ya kila uchao yanazidi kuwaondelea matumaini raia wa taifa hilo la Mashariki ya Kati.
  2. Baada ya janga la COVID-19 kufichua ni kwa kiasi gani jamii ilikuwa haipatii wafanyakazi muhimu thamani wanayotakiwa ikiwemo malipo ya kutosha na mazingira bora ya kazi, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO limetoa ripoti inayosihi nchi zote duniani ziboreshe mazingira ya kazi ya watendaji hao.
  3. Makala tunakupeleka nchini Bahrain katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manama ambako mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani ulioanza tarehe 11 mwezi huu wa Machi umehitimishwa leo tarehe 15. Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson ambaye ni Rais wa Kundi la Kijiografia na Kisiasa la Mabunge ya Afrika amezungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuhusu mambo kadhaa ikiwemo waliyoyajadili katika Mkutano huo.
  4. Na mashinani tunakupeleka Geneva, Uswisi kwa Neema Lugangira mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mradi bingwa wa kutumia TEHAMA kuboresha afya na lishe miongoni mwa wazee.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
13'15"