Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 FEBRUARI 2023

20 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani linaangazia lugha ya mama tunapoelekea katika siku ya Lugha ya Mama Duniani, na huduma za afya nchini Syria baada ya tetemeko la ardhi.  Makala tutakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Uganda.

  1. Kuelekea siku ya kimataifa ya lugha mama duniani hapo kesho, mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu makabila madogo amesema serikali lazima zichukue hatua zaidi juu ya matumizi ya lugha za makabila hayo madogo kwani zama za kuchagua lugha moja tu kutumiwa na taifa zima huku nyingine zikienguliwa zimepitwa na wakati.
  2. Ujumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa umetembelea hospitali na kliniki zinazoungwa mkono na shirika lisilo la kiserikali la Misaada na Maendeleo la Syria au SRD, Kaskazini Magharibi mwa Syria na kujionea athari za tetemeko la Ardhi lililoikumba nchi hiyo wiki mbili zilizopita pamoja na kujionea usambazaji wa misaada iliyotolewa na Umoja wa Mataifa.
  3. Katika makala tunaelekea kaskazini magharibi mwa Tanzania katika eneo la Mugumu, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kuangazia harakati za shirika la Hope For Girls and Women in Tanzania kupigania haki za kijamii.
  4. Na katika mashinani tutaelekea wilayani Kaabong nchini Uganda kupata ushauri kutoka msichana muathirika wa mimba za utotoni.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'4"