Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 FEBRUARI 2023

15 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia kazi za Umoja wa Mataifa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi, na pia kazi za umoja huo nchini Ukraine. Makala tunakupeleka nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Wakati vita nchini Ukraine ikikaribia kuingia mwaka wa pili, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo kwa pamoja wameomba jumla ya dola bilioni 5.6 ili kupunguza madhila yanayowakabili mamilioni ya watu walioathirika na vita nchini Ukraine.
  2. Mkuu wa kanda ya nchi za kiarabu katika shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu duniani, na afya ya uzazi, UNFP Leila Baker amesema pamoja na shirika hilo kuhitaji fedha ili kuweza kuwahudumia wanawake na wasichana waliathiriwa na matetemeko nchini Turkiye na Syria lakini kila sehemu anapopita nchini Syria wanawake hutoa ombi moja tu nalo ni kuhitaji amani.
  3. Katika makala Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaendelea na hatua zake za kuhakikisha wakimbizi waliorejea nyumbani wanaishi maisha ya utu na ustawi, ambapo pamoja na kuwapatia wakimbizi hao huduma bora pia linazidi kuomba wahisani waoneshe ukarimu zaidi.
  4. Na katika mashinani tutaelekea nchini Tanzani kusikia njia mbadala na fimbo za kuleta nidhamu shuleni. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'11"