Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 FEBRUARI 2023

08 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakwenda mashariki ya kati na nchini Ukraine. Makala tutaelekea nchini Tanzania na mashinani tutasikia ujembe wa mchehemuzi wa vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na pia mwanasayansi.

  1. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa muda wa Misaada ya Kibinadamu nchini Syria El- Mostafa Benlamlih amesema ingawa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada wanafanya kila juhudi kusaidia wananchi walioathiriwa na matetemeko ya ardhi lakini hali ni mbaya kwani hawapati msaada ya kutosha.
  2. Mwishoni mwa mwezi huu wa Februari tarehe 24, utatimia mwaka mmoja tangu uvamizi wa sasa wa Urusi kwa Ukraine. Nchini Ukraine, moja ya sekta zilizoathiriwa sana na vita hii ni kilimo Anold Kayanda anamwangazia mkulima mmoja katika mkoa wa Odesa kusini magharibi mwa nchi. 
  3. Makala tunakwenda mkoani Njombe nchini Tanzania kutathmini harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO za kuchagiza kilimo cha bustani kikijumuisha kilimo cha mikunde kama njia mojawapo ya kuimarisha afya na ustawi wa jamii.
  4. Na katika mashinani Gitanjali Rao, Mchehemuzi wa vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na pia mwanasayansi  anatoa maoni yake kuhusu nini kifanyike ili kuwapa wasichana na wanawake fursa nyingi za masomo na kazi katika sekta ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, au STEM.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'46"