Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 FEBRUARI 2023

06 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazi siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana, FGM na kazi za UNICEF nchini Yemen.

  1. Hii leo ni ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka wanaume na wavulana wapaze sauti zao kusaidia kutokomeza mila hiyo potofu na hatarishi.   
  2. Huduma za kujisafi na usafi mara nyingi husalia ndoto kwa wakimbizi wa ndani kwa kuwa kipaumbele kinakuwa ni usalama wao hali inayoongeza zaidi hatari ya kupata magonjwa iwapo wanakosa huduma hizo na ndio maana nchini Yemen, Umoja wa Mataifa umechukua hatua kuwezesha wayemen waishio kambini wanaweza kujikinga pia na magonjwa yatokanayo na uchafu. 
  3. Makala ni kuhusu siku hii ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji tumsikilize Robi Samuel Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania lenye makao yake makuu Mgumu wilayani Serengeti mkoani Mara likijishughulisha pamoja na mambo mengine kupambana dhidi ya mila iliyopitwa na wakati ya ukeketaji, yeye mwenyewe akiwa mmoja wa manusura wa tendo hilo la kikatili anaeleza siku hii ya kimataifa ina maana gani kwake
  4. Na katika mashinani tunasilia na siku ya kutokomeza ukeketaji na tutasikia ujumbe kutoka kwa balozi mwema wa shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'18"