Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya Benet nchini Uganda yaiomba utaifa: UNHCR

Jamii ya Benet nchini Uganda yaiomba utaifa: UNHCR

Pakua

Baada ya zaidi ya takriban miongo minane ya kutokuwa na utaifa, jamii ya watu wa asili ya Benet nchini Uganda inahaha kuishi, na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bila kuwa na nyaraka rasmi muhimu jamii hiyo haiwezi kupata huduma za msingi kama elimu na afya , na sasa jamii hiyo inaiomba serikali ya Uganda kumaliza zahma hiyo iliyowaghubika kwa miongo.

Huyo ni mzee Moses Kapchekwengu mmoja wa watu wa jamii ya asili ya Benet inayoishi kwenye msitu wa mlima Elgon Uganda akisema , mtihani wao ulianza wakati Waingereza walipokuja  na walifanya eneo lao lote kuwa hifadhi ya msimu mwaka 1936 na 1937, na jamii ya Benet ikasalia bila ardhi. 

Moses anaendelea kusema kwamba mahali hapo ndipo walipiozaliwa na kukulia na hawa pengine wanapopaita nyumbani zaidi ya hapo, “Tulikuwa tunaishi katika ardhi hii , tanghu jadi tumekuwa tunaishi happ na watu wengine walikuwa wanaishi mbugani, mbugani ni Kusini mwa hifadhi hiyo” 

UNHCR inasema jamii ya Moses ni wafugaji na wamekuwa hapa kwa karne kadhaa lakini hawatambuliki kama raia. Moses anasema,  “Matatizo yakaanza kwani sasa hatukuwa na radhi tena, hatukuweza kupata chakula pia hatukuweza tena kupata fursa ya huduma nyingine za kiuchumi na kijamii kama shule, barabara na vitu vingine tangu wakati huo. Lakini sasa kibaya zaidi ni kwamba hawatutilii maanani, wametusahau.” 

Hivi sasa UNHCR na wadau wanafanyakazi na serikali ili kusaidia jamii kama ya Benet kwani ni dhahiri shairi kuwa bila uthibitisho wa vitambulisho hawawezi kupata huduma muhimu.  

David Mande ni mratibu wa program ya jamii ya walio wachache ya watu wa wasili wa Benet anasema bila nyaraka ni mtihani mkubwa “Wakati mwingine nataka kupata fursa ya huduma mfano mkopo benki lakini siwezi kwa sababu sina kitambulisho cha taifa, wakati mwingine najiuliza na nahisi nataka kukimbia kama wengine wanavyofanya, lakini siwezi kwasababbu sina na siwezi kupata pasi ya kusafiria” 

Viola Kopok yeye ni mkunga wa jadi , na hana kitambulisho rasmi na kwa ajili hiyo kujikimu kimaisha ni changamoto kubwa na pia  kutoa huduma ambayo wanawake wengi wanaihitaji katika jamii yake, anasema “Hatuna fursa ya vituo vya afya hivyo kupewa rufaa Kwenda huko ni ngumu. Mungu akikubariki na kilo ya unga basi unampa mwanamke aliyejifungua, na wengi wetu hulala njaa”. 

Kutokuwa na utaifa kulingana na UNHCR ni hali yenye athari nyingi kwa familia na jamii kutoka vizazi hadi vizazi na mantiki hiyo inasema  jamii ya Benet ina haki ya kutambulika katika eneo hilo. 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
3'6"
Photo Credit
UNHCR Video