Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante Katibu Mkuu kwa kuendelea kuniamini: Elizabeth Mrema

Asante Katibu Mkuu kwa kuendelea kuniamini: Elizabeth Mrema

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumanne wiki hii alimtangaza Elizabeth Maruma Mrema kutoka nchini Tanzania kuwa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP

Bi Mrema tangu mwaka 2020 amehudumu kama katibu mtendaji wa sekretarieti ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai CBD, yenye makao yake makuu mjini Montreal, Canada akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili baada ya uteuzi huo ameelezea alivyoupokea 

(SAUTI YA ELIZABETH MREMA) 

“Kwanza ni furaha kubwa sana kwangu kwa Katibu Mkuu kuniamini , kunipa kazi hii na pili namshukuru Mungu kwa baraka zake kunifikisha hapa mahali na kuweza kupewa hii kazi muhimu. Nahakika kulikuwa na wengi hapa ulimwenguni ambao ni wataalam zaidi kuliko mimi lakini Katibu Mkuu amenichagua mimi anajua ni kwa sababu gani na anajua bila shaka labda sitamuangusha n ani kwa sababu pia ameshanipa madara kama haya katika sehemu nyingine na nimeweza kutenda vizuri. Namshukuru sana kwa Imani hiyo na namshukuru sana kwa kuniona kwamba katika hao wengi naweza kuifanya hii kazi.” 

Na nini basi dunia ikitarajie kutoka kwake katika wadhifa huu mpya 

(SAUTI YA ELIZABETH MREMA) 

“Kwanza nafikiri ni muhimu kukumbuka kwamba mtu yeyote anayefanya kazi kwenye Umoja wa Mataifa na mimi nikiwa mmoja wapo hasa nikiwa kiongozi wa ngazi za juu nisipendelee nchi yeyote, au nisipendelee mtu yeyote kwa sababu nchi zote ziko saw ana natakiwa nisiegemee kokote. Kwa hivyo nategemea kusaidia nchi zote sawasawa lakini vilevile watu wakumbuke kwamba shirika la mazingira linatoa misaada mingi sana hasa kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwa moja wapo, pia labda ndio kuna matatizo mengi sana ya mazingira.” 

Bi. Mrema akaenda mbali zaidi na kusema mshikamano na nchi zinazoendelea ni muhimu sana 

(SAUTI YA ELIZABETH) 

“Nchi ambazo zimekwishaendelea zinatusaidia kwa ajili ya kupata teknolojia, kupata wataalam pamoja na kufadhili miradi mingi inayohusu mazingira kwenye nchi zinazoendelea. Mimi nikiwa nimetoka Tanzania, Afrika pia ni kwenye maeneo ya nchi zinazoendelea ni kweli kwamba muda wangu mwingi utakuwa ni kusaidia hizi nchi kwa sababu ndio zinazosaidiwa zaidi katika shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, kwa hiyo sitaonekana kuwa napendelea nikifanya hivyo. Kwa hiyo nashukuru na nategemea kwamba nitafanyakazi inavyotakiwa na kusaidia nchi kama inavyotakiwa ili mazingira yetu ya dunia angalau yabadilike.” 

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'37"
Photo Credit
UN News