Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TANZBATT 6 wakabidhiwa jukumu la ulinzi wa amani wa UN nchini CAR

TANZBATT 6 wakabidhiwa jukumu la ulinzi wa amani wa UN nchini CAR

Pakua

Kikosi cha 5 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANZBATT 5 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, kimekamilisha muda wake  na kukipisha kikosi kingine cha 6 nacho kutoka Tanzania, TANZBATT 6 ambacho kitaendeleza jukumu hilo. Kutoka Berberat, Captain Mwijage Inyoma ni Afisa Habari wa TANZBATT 06 ametuandalia taarifa hii. 

Mwaka mmoja wa pilika za kuhamasisha amani, mshikamano na kuitunza amani umekamilika kwa kikosi cha wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 5 yaani TANZBATT 5 na wanaondoka wakifurahi kwamba wametoa mchango wao kwa amani ya ulimwengu kupitia Umoja wa Mataifa.  

Luteni Kanali Kiiza ni Kamanda Kikosi kinachoondoka anasema,  

(Sauti/Video ya Lut Col Kiiza) 

Kwa upande wake Mkuu wa TANZBATT 6 ambao ndio wanaolipokea jukumu hilo la ulinzi wa amani, Luteni Kanali anaeleza mikakati aliyonayo....

(Sauti/Video ya Lut Col Mshana) 

Mmoja wa raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mkazi wa mjini Beriberati kwa niaba ya wengine anatoa shukrani kwa walinda amani  

(Sauti ya raia) 

Kutoka Berberat, Mambere Kadei, ni Kapteni Mwijage Inyoma, TANZBATT 06. 

Audio Credit
Kapteni Mwijage Inyoma
Audio Duration
2'35"
Photo Credit
Meja Asia Hussein