Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutanguliza majadiliano katika kutatua matatizo ya ukosefu wa amani utarejesha amani DRC: Meja Jenerali Simuli

Kutanguliza majadiliano katika kutatua matatizo ya ukosefu wa amani utarejesha amani DRC: Meja Jenerali Simuli

Pakua

Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli ambaye ni Mkuu wa Utumishi katika Jeshi la Tanzania ametoa wito kwa Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kutanguliza majadiliano katika kutatua matatizo yao ya ukosefu wa amani. 

Meja Jenerali Simuli ametoa wito huo alipoongoza ujumbe wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika ziara yao nchini DRC ili kujionea shughuli za mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO ambamo kwa nyakati tofauti, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wamekuwa wakihudumu katika vikosi mbalimbali kikikwemo cha kujibu mashambulizi, FIB. 

Kwanza alihudhuria hafla ya kuwavisha nishani za Umoja wa Mataifa askari wa Tanzania wanaolinda amani nchini DRC. 

Nats.. 

Kisha wito wake kwa raia wa DRC, 

Sauti ya Meja Jenerali Simuli..

“Mimi ujumbe ambao ningeweza kuwapa wacongoman (Raia wa Congo), kama ndugu zangu, kaka zangu, dada zangu, waafrika wenzangu, ni kwamba matatizo yakijitokeza basi wakae mezani kwa pamoja na kuyazunumza kwa pamoja na kupata kile ambacho wanakihitaji. Kwa sababu ili nvhi iendelee inahitaji amani. Mkitulia mtakwenda mbele sana. Na nchi ya DR Congo nina Imani wananchi wakikaa vizuri, wakiacha munkari, yaani wakiacha hasira, wakakaa mezani na kuzungumza, matatizo yatakwisha.”  

Na je Meja Jenerali Paul Simuli ana ujumbe gani kwa walinda amani? 

Sauti ya Meja Jenerali Simuli..

“Walinda amani ninawaomba waelekee kwenye yale majukumu ambayo wamekuja kuyatekeleza hapa kwa wenzetu (DRC). Kwa sababu jambo lao kubwa ni kuwalinda wananchi ambao wanapata madhara.” 

Audio Credit
Anold Kayanda/Meja Jenerali Paul Simuli
Sauti
1'46"
Photo Credit
TANZBATT_8/Kapteni Tumaini Bagambo