Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 NOVEMBA 2022

03 NOVEMBA 2022

Pakua

 

Hii leo katika Habari za UN tunakuletea Mada kwa Kina, Habari kwa Ufupi na Methali ni mwanzo kokochi, mwisho nazi.

 

  1. Mada kwa Kina: Inajikita Rwanda ambako Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alishiriki Umuganda ambao ni mradi wa kijamii wa uhifadhi wa mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Shughuli ilifanyika Kigali, mji mkuu wa Rwanda.
  2. Habari kwa Ufupi:
  • Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema miezi miwili tangu mafuriko yakumbe Pakistani, watoto zaidi ya milioni 2 hawajaweza kwenda shule kwa sababu shule zao haziingiliki baada ya mafuriko kuharibu takribani shule elfu 27 nchini humo.
  • Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP Kanda ya Pembe ya Afrika Michael Dunford amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kusema kwa kipind icha miezi sita ijayo, watahitaji dola bilioni 2.1 kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya wakazi wa eneo hilo waliokumbwa na ukame uliodumu kwa miongo minne sasa.
  • Na Umoja wa Mataifa umeonya hii leo kuwa njaa na utapiamlo vinaongezeka katika maeneo yote yaliyokumbwa na mafuriko, ukame na mizozo nchini Sudan Kusini huku naadhi ya jamii zikiwa hatarini kukumbwa na njaa iwapo misaada ya kibinadamu haitakuwa endelevu, halikadhalika mikakati ya kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi haitaimarishwa.
  1. Methali: Mwanzo kokochi, mwisho nazi na mchambuzi ni Josephat Gitonga, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kitengo cha Utafsiri na Ukalimani.

 

Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
13'12"