Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi wapewa vyeti vya kuzaliwa Tanzania

Wakimbizi wa Burundi wapewa vyeti vya kuzaliwa Tanzania

Pakua

Asante Tanzania mwanangu sasa atajulikana alipozaliwa :Mkimbizi Evangeline 
Familia za wakimbizi wa Burundi wanaoishi kwenye kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma nchini Tanzania wameishuru serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki kwa kuwapatia nyaraka muhimu za watoto wao, vyeti vya kuzaliwa wakati wa ziara ya Kamisha Mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi iliyokamilika mwishoni mwa wiki. Happiness PPalangyo na taarifa zaidi

(TAARIFA YA HAPINESS PALANGYO)
Katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Kigoma familia hizi za wakimbizi zinafurahia kitu ambacho wengi wanakiona cha kawaida kabisa na hawakitilii maanani, vyeti vya kuzaliwa . Miongoni mwa waliokabidhiwa vyeti hivyo na kamishina mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi wakati wa ziara yake Kigoma ni Evangeline mkimbizi kutoka Burundi ambaye anasema  

“Nyaraka hizi zitanisaidia kuonyesha wapi watoto wangu walipozaliwa na pia zitawasaidia kupata msaada” 

Wakati wa ziara yake kambini hapo Grandi na wazazi hao wamekaribisha hatua hiyo ya Tanzania ya kuwasaidia kupata nyaraka muhimu ili waweze kupata huduma za msingi nchini humo, na siku moja watakaporejea nyumbani .

Angelene anasema hadi sasa  “Tayari nimeshapokea vyeti viwili vya kuzaliwa vya watoto wangu na nasubiri cha mtoto wa tatu.” 

Kwa upande wake Grandi amesisitiza kuwa “Kwa watoto wanaozaliwa ukimbizini kutokuwa na cheti cha kuzaliwa kunaweza kuwatumbukiza katika janga la kutokuwa na utaifa wakikua. Pia katika hali ya kusafirishwa hiki ni kitu kimoja muhimu. Ni muhimu sana wao kurejea nyumbani na kuwa na kitu kinachothibitisha utambulisho wao.” 

Tanzania imekuwa ikikaribisha na kukikirimu wakimbizi kwa miongo mingi na hivi sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi 240,000 wengi wakiwa ni kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC. 

Audio Credit
Flora Nducha / Hapiness Palangyo
Audio Duration
2'1"
Photo Credit
UNHCR/Georgina Goodwin