Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwani haribifu wageuzwa tofali Mexico

Mwani haribifu wageuzwa tofali Mexico

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP nchini Mexico linafadhili miradi ya maabara za wabunifu wanaopatia majawabu changamoto za kijamii zitokanazo na  matatizo yanayowazunguka. Miongoni mwa miradi hiyo ni ule wa kusafisha fukwe za bahari na uchafu unaokusanywa ukiwemo mwani aina ya Sargusssum, kutumika kutengeneza nyumba. Tupate undani wa taarifa hii iliandaliwa na UNDP na kusomwa studio na Evarist Mapesa wa Redio washirika SAUT FM.
Maji yakipiga fukwe ya baharí ya Riviera Maya, maji hayo ya bahari yanakuja na lundo la mwani na mfanyabiashara Omar Sánchez aliona fursa ya kufanya usafi na mwaka 2015 aliingia mkataba na hoteli zilizopo ufukweni kwa ajili ya kusafisha, mkataba ambao uliwanufaisha takriban familia 300 zilizopata ajira ya kusafisha mwani huo wa Sargassum. 
Sánchez anasema “Tatizo la mwani wa sargassum ni kubwa. Kwa uzoefu wangu, nimeliona likikua na kukua na kukua kila mwaka.”
Mfanyabiashara huyo alikuwa akikusanya na kutupa mwani huo lakini baada ya kujiunga na maabara ya UNDP inayolenga kuongeza kasi ya suluhisho zinazobuniwa na wanajamii ndipo alipopata wazo la kutotupa mwani wa Sargassum bali kuuchakata na kutengeneza matofali ya kujengea nyumba na kuyapa jina la Sargablock.
Sánchez nasema historia yake ndio ilimsukuma kupata wazo la matofali hayo wakati akiwaza kutafuta mbinu bora za kuisaidia jamii “ jambo la kwanza nililofanya ni kujiweka katika viatu vya wengine. Mama yangu alikufa na hakuwahi kuwa na nyumba yake mwenyewe. Kwa hivyo, nina nini kwa 'Casa Angelita'? Kwanza, nikafikieia wengine na kuanza na wazo la nyumba. Kutokuwa na nyumba ni kejeli ya maisha: Mimi nimekuwa bila makao na sasa nimepata fursa hii ya kusaidia watu wengine.”
Kampuni yake kwa siku inauwezo wa kutengeneza matofali 1,000 na maono haya ya Sanchez yanamuwezesha kutoa nyenzo ya ujenzi wa gharama nafuu, kujenga nyumba za bei nafuu kwa wakazi wa eneo la Riviera Maya na kutimiza kiu ya familia nyingi ya kuishi katika nyumba zao wenyewe kwa staha.
 
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Evaris Mapesa
Audio Duration
2'12"
Photo Credit
UN News/ Conor Lennon