Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yahitaji 'kijiji' kusaidia walio kwenye majanga - Guterres

Yahitaji 'kijiji' kusaidia walio kwenye majanga - Guterres

Pakua

Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya utoaji wa misaada ya kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepazia sauti watoa huduma za kibinadamu ambao hufanya kazi kutwa kucha a hasa kwa wale wanaopitia majanga wanaojikuta wao wenyewe wakibeba jukumu la kutoa msaada ili dunia iwe pahala bor
 
Katika ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video hii leo, Katibu Mkuu ametumia methali isemayo yahitaji Kijiji kukuza mtoto, akiongeza kuwa yahitaji pia Kijiji kusaidia watu wanaokumbwa na majanga ya kibinadamu. 
“Kijiji hiki kinajumuisha waathirika ambao kila wakati wao ndio wa kwanza kuchukua hatua pale janga linapotokea; majirani wakisaidia majirani. Inajumuisha jamii ya kimataifa inaungana kusaidia watu hao wakati wanajikwamua na kujijenga upya.” 
 
Amesema wengine ni mamia ya maelfu ya watu binafsi watoa misaada wakiwemo wanaojitolea na watu wabobevu kwenye tasnia zao wakitoa huduma za afya na elimu, maji na chakula, malazi na ulinzi, msaada na matumaini. 
 
Katibu Mkuu amesema watoa misaada hao huweka maisha yao rehani wakitekeleza majukumu hayo katika maeneo hatari zaidi hata kuweza kufikirika. 
 
“Leo hii idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu imekuwa kubwa kuliko kwa sababu ya mizozo, mabadiliko ya tabianchi, COVID-19, umaskini, njaa na kiwango kisicho cha kawaida cha ukimbizi wa ndani. Katika siku ya leo ya usaidizi wa kibinadamu, hebu na tuwafurahie wasaidizi wa kibinadamu kokote waliko. Ujasiri wao, na tuwakumbuke wale waliopoteza maisha wakitekeleza jukumu hilo la kiutu » 
 
 
Siku ya usaidizi wa kibinadamu duniani ilitengwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2008 kufuatia shambulio la ofisi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad, Iraq mwaka 2003, shambulio lililoua wahudumu wa kibinadamu 22. 
 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'3"
Photo Credit
© UNOCHA/Matteo Minasi