Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusisubiri kujenga ukuta Somalia, bali tuzibe ufa! Yasema FAO ikitaka Somalia isaidiwe sasa badala ya kusubiri hali iwe mbaya

Tusisubiri kujenga ukuta Somalia, bali tuzibe ufa! Yasema FAO ikitaka Somalia isaidiwe sasa badala ya kusubiri hali iwe mbaya

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limetoa ombi la dola zaidi ya dola milioni 131ili kusaidia wananchi 882,000 kutoka wilaya 55 nchini humo wenye uhitaji wa haraka wa msaada wa kuokoa maisha yao kutokana na ukame unaokabili taifa hilo la pembe ya Afrika. FAO imesema jumuiya ya kimataifa isisubiri hadi baa la njaa litangazwe nchini Somalia ndio hatua zichukuliwe na badala yake imetaka misaada ya kimkakati ianze kutolewa sasa. Leah Mushi ana habari kamili.
Uti wa mgongo wa taifa la Somalia ni kilimo kinachotegemewa kwa takriban asilimia 60 kuendesha Maisha ya wananchi waweze kujipatia chakula na kile wanachouza waweze kujikimu, lakini mabadiliko ya tabianchi yaliyoleta ukame mkali nchini humo yamesababisha zaidi ya wananchi 900,000 wengi kutoka vijijini kuyakimbia makazi yao kusaka misaada katika kambi za wakimbizi wa ndani tangu mwezi Januari mwaka jana 2021 ili angalau waweze kupata chakula na kuweza kuishi.
Mkurugenzi wa FAO anayehusika na dharura na mnepo Rein Paulsen hivi karibuni ametembelea nchini humo kujionea hali halisi na pia kuzungumza na wakimbizi wa ndani walio katika makambi ambao wengine wamemueleza mifugo yao imekufa sababu ya ukame na kutembea zaidi ya kilometa 100 kutafuta msaada kambini hapo.
Paulsen amesema ili kutatua changamoto nchini Somalia lazima kuanza kutibu kwenye mzizi wa tatizo
“Mwitio wa tatizo la njaa uanzie maeneo ya vijijini, huko ndio kwenye kitovu cha tatizo ambapojumuiya za wazalishaji wa chakula wameathirika na ukame mkali. Hatuwezi kusubiri mpaka njaa itangazwe, lazima tuchukue hatua sasa ili kusaidia watu kupata riziki na kuweza kuishi.”
Akizungumzia kuhusu muitikio wa watu kuchangia misaadda ya kibinadamu amesema “Ufadhili umeendelea kuwa mdogo mpaka kufikia jana Agosti 4,2022 ni asilimia 43 pekee ya ufadhili imepatika.” Hii ikiwa saw ana asilimia 46 ya ufadhili unaohitajika nchini Simalia.
Mkurugenzi huyo wa dharura wa FAO amesema kwa ufadhili waliopata mpaka sasa wameweka nguvu zaidi katika kutoa fedha taslimu ili watu waweze kununua chakula na kujikimu, kulisha mifugo yao , kuwapatia maji safi na salama na kupatia matibabu mifugo yao. “Licha ya changamoto ya uhaba wa mvua, tunahakukisha tunafikisha msaada kwa wakulima ili waweze kupanda pale inapowezekana, kilimo cha umwagiliaji kinawezekana. Hivi ndio aina za misaada ya vitendo inayohitajika”.
FAO nchino Somalia imetoa ombi hilo la dola milioni 131.4  lengo kuu ikiwa ni kuongeza utoaji wa misaada vijijini ili kuwasaidia watu wasiojiweza pale walipo. “Huu ni ufanisi zaidi, ubinadamu zaidi na nilazima kwa pamoja tuongeze juhudi kwakuwa kiwango cha msaada kilichotolewa sasa hakitoshi kwahiyo tunahitaji mwitikio wa msaada kutoka katika kila sekta ili kusaidia Maisha ya watu.”
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Leah Mushi
Audio Duration
3'1"
Photo Credit
FAO