Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Meli ya kwanza ya Shehena kutoka Ukraine yakamisha ukaguzi nchini Uturuki na kuanza safari kuelekea Lebanon

Meli ya kwanza ya Shehena kutoka Ukraine yakamisha ukaguzi nchini Uturuki na kuanza safari kuelekea Lebanon

Pakua

Meli ya kwanza ya Ukraine iliyobeba shehena ya tani 26,000 za mahindi kwenda kuuzwa nchini Lebanon imekamilisha ukaguzi wake nchini Uturuki na kuruhusiwa kuendelea na safari yake hii leo. 

(Taarifa ya Leah Mushi) 

Meli hiyo MV Razoni iliondoka Bandari ya Odesa nchini Ukraine tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti ikiwa ni kuanza utekelezaji wa Makubaliano ya Mpango wa Nafaka katika Bahari Nyeusi ulioruhusu nchi hiyo kusafirsha nafaka kwa sharti la meli zote kupita Instabul, Uturuki na kukaguliwa na kikosi kazi maalum ili zisibebe silaha na magendo wakati zinaenda na zinaporudi katika soko la Kimataifa.

Kikosi cha ukaguzi kinajumuisha wakaguzi kutoka Umoja wa Mataifa, Urusi, Uturuki na wenyewe Ukraine ambao kwa pamoja mbali na kukagua mzigo pia wanakagua wafanyakazi walio melini kabla ya kuruhusu kuendelea na safari.

Meli hii ya kwanza yenye  tani elf 26 za mahindi kupeleka mji wa bandari wa Tripoli nchini Lebanon inaelezwa kuwa ni muhimu zaidi kwa kuwa ukaguzi huu wa kwanza ndio utatumika kama msingi na mfano wa kaguzi nyingine zote zitakazoendelea za meli kutoka Ukraine ambayo kwa sasa ipo kwenye mzozo na Urusi hali iliyofanya nchi hiyo ishindwe kusafirisha nafaka tangu mwezi Februari mwaka huu Ukraine ilipovamia Urusi.

Katibu Mkuu ww Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mwezi Aprili mwaka huu alizuru nchi hizo mbili na kuzungumza na viongozi wake, mazungumzo ambayo yalizaa matunda ya mkataba wa Mpango wa Nafaka katika Bandari Nyeusi mwishoni mwa mwezi Julai.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeleta madhara kwa nchi zote duniani hususan za kipato cha chini kwa kuongezeka kwa gharama za bidhaa, mbolea na mafuta .

Audio Credit
Assumpta Massoi / Leah Mushi
Audio Duration
1'44"
Photo Credit
OCHA/Saviano Abreu