Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali mwanzoni ilikuwa mbaya sasa UNHCR imetusaidia- Mkimbizi DRC

Hali mwanzoni ilikuwa mbaya sasa UNHCR imetusaidia- Mkimbizi DRC

Pakua

Hali si shwari kwa makumi ya maelfu ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutokana na kuendelea kufurushwa makwao kutokana na ghasia zinazochochewa na vikundi vilivyojihami mashariki mwa nchi hiyo. Mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka kila uchao huku ufadhili kwa mashirika kama lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ukipungua.

Lakini shirika hilo linajitahidi kuwapatia wakimbizi msaada wa kimkakati ili waweze kujitegemea. Wako walionufaika na wengine wanahitaji usaidizi zaidi kwa watoot wao waweze kwenda shuleni.

Hali iko vipi kwa tamu na chungu hiyo? Ungana basi na Ibrahim Rojala wa Televisheni washirika Mamlaka TV kutoka Tanzania akisimulia makala hii iliyoandaliwa na UNHCR. 

 

Audio Duration
3'58"
Photo Credit
© UNOCHA/Endurance Lum Nji