Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sawa Wanawake Tanzania lasongesha haki za mtoto Morogoro, Tanzania 

Sawa Wanawake Tanzania lasongesha haki za mtoto Morogoro, Tanzania 

Pakua

Nchini Tanzania mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yanaendelea kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa za kufanikisha mikataba ya kimataifa ikiwemo ule wa haki ya mtoto unaotaja haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni Kuishi, Kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa. 

Miongoni mwa mashirika hayo ni SAWA Wanawake Tanzania ambalo linatambua umuhimu wa mtoto kuendelezwa kwa kupatiwa elimu na wakati huo huo kulindwa dihdi ya vitendo vya ukatili. Harakati za hivi karibuni zaidi za shirika hilo ni katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambako shirika hilo liliandaa bonanza kuelimisha jamii kuhusu haki na ulinzi wa mtoto, ikisisitizwa kuweka mbele suala la malezi bora kwa wtoto, kuwalinda na ukatili ikiwemo wa kingono ili awewe kuhitimu masomo yake na kutimiza Ndoto kwani kata ya Dakawa inahitaji msaada kuwanusuru watoto. 

Nini kilifanyika? Hamad Rashid wa Radio washirika Kids Time FM nchini humo ameshuhudia bonanza hilo na kuandaa Makala hii. 

Audio Credit
Leah Mushi/Hamad Rashid
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
© UNICEF/Shehzad Noorani