Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania walenga kuhamasisha amani DRC kupitia Kiswahili 

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania walenga kuhamasisha amani DRC kupitia Kiswahili 

Pakua

Kikundi cha tisa cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-9, kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimeanza kusambaza daftari na vifaa vingine vya shule kwa watoto katika maeneo ya Mavivi huko BENI mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kuwahimiza wanafunzi hao kuzungumza lugha ya Kiswahili ili wakimaliza shule waweze kuwasiliana na mataifa mengine. Hii imekuja wiki chache tu baada ya kusherehekewa (nimondoa kushereekewa) kwa Siku ya Kiswahili Duniani ambayo iliadhimishwa tarehe 7 mwezi huu Julai. Mwandishi wetu wa DRC Byobe Malenga ametuandalia makala ifuatayo. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Byobe Malenga
Audio Duration
4'27"
Photo Credit
TANZBATT9